29 Apr

Bilion 4.1 zakusanywa kugharamia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupitia Taasisi isiyo ya kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) wafanya harambee kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Harambee hiyo imefanyika Novemba 3, 2024 katika Hoteli ya Johari Rotana iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 4.1 zilikusanywa kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto.