HTAF yashiriki Female Future Alumni Networking Cocktail Dinner ya ATE Dar es Salaam, 24 Octoba 2025
Taasisi ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) imeshiriki katika hafla ya Female Future Alumni Networking Cocktail Dinner iliyoandaliwa na Association of Tanzania Employers (ATE), hafla ambayo imefanyika katika hoteli ya Sea Cliff, jijini Dar es Salaam, chini ya uongozi wa Bi. Suzan Ndomba, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE. Katika hafla hiyo yenye lengo la kuwakutanisha washiriki na wahitimu wa programu ya Female Future, HTAF iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dkt. Naizihijwa Majani, Pamoja na Managment ya HTAF Dkt. Majani, ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu (main speaker) wa hafla hiyo, alitoa mada yenye kuelimisha juu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake na watoto, akibainisha changamoto zinazowakabili wanawake na watoto wengi wenye matatizo ya moyo nchini, pamoja na umuhimu wa uchunguzi wa mapema na huduma za matibabu ya kitaalamu. Aidha, alieleza kwa undani jinsi Heart Team Africa Foundation (HTAF) inavyotekeleza majukumu yake kwa kugusa mioyo ya jamii kupitia huduma za afya, elimu, na kampeni za uhamasishaji, akisisitiza kauli mbiu ya taasisi hiyo inayolenga “kugusa mioyo na kuleta matumaini kwa watoto.” Dkt. Majani alitumia fursa hiyo pia kuwahamasisha wanawake waliohudhuria kuendelea kutumia nafasi zao katika uongozi na jamii kusukuma mbele ajenda za afya, hususan katika kulinda vizazi vijavyo kupitia huduma bora za moyo kwa watoto.