Heart Team Africa Foundation

Heart Team Africa Foundation

In the joy of others lies our own

03 Dec

Heart Team Africa Foundation yatambua mchango wa NMB katika kuokoa maisha ya watoto

Heart Team Africa Foundation (HTAF) imetambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na Benki ya NMB katika kusaidia juhudi za kuokoa maisha ya watoto wanaohitaji matibabu maalum ya afya, hususan huduma za matibabu ya moyo. Tangu kuanza kwa ushirikiano huo, NMB imeweza kuchangia jumla ya Shilingi milioni 500, kiasi ambacho kimewezesha watoto 125 kupata matibabu na huduma muhimu za kuokoa maisha. Katika Ziara hiyo iliyofanywa na NMB bank. Mtendaji Mkuu wa HTAF, Dkt. Naizihijwa Majani (kushoto), alimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, zawadi maalum kama ishara ya shukrani kwa mchango na ushirikiano wa benki hiyo katika kuboresha afya za watoto nchini. HTAF imeeleza kuwa msaada wa NMB umekuwa nguzo muhimu katika kufanikisha programu za matibabu ya moyo kwa watoto, pamoja na kuimarisha huduma za afya zinazolenga kuokoa maisha ya watoto.

recent news